Thursday, July 31, 2025

SIRI ZA MTI WA MWEMBE KIROHO

 

๐ŸŒฟ Dr Magowo ๐ŸŒฟ

๐Ÿ”ฅ SIRI ZA MTI WA MWEMBE KIROHO ๐Ÿ”ฅ

Mti wa mwembe si wa matunda tu — una siri nzito za kiroho zilizofichwa tangu enzi.


๐ŸŒŒ TIBA ZA KIROHO ZA MWEMBE

✅ 1. Kuvunja Agano la Ukoo

Mti wa mwembe ni mti wa agano kwenye mila nyingi. Wachawi hutumia majani yake kutengeneza maagano ya damu au viapo vya kifamilia.
๐Ÿ”“ Kukata tawi la mwembe kwa maombi ya kuvunja agano husaidia kuachilia kizazi kutoka mikataba mibaya.


✅ 2. Kufuta Alama za Kipepo au Vitu Ulivyolishwa Ndoto

Watu wanaolishwa vyakula ndotoni au kunyweshwa usiku kiroho, hufaidika kwa kuchemsha majani ya mwembe na kuoga nayo kwa siku 3–7.
๐Ÿ’ง Husaidia kutapika kiroho yale yaliyoingizwa ndani ya mwili.


✅ 3. Kusafisha Maeneo Yenye Historia ya Uchawi

Nyumba zilizo karibu na miembe mikubwa hutumika sana na wachawi usiku.
๐Ÿงน Majani ya mwembe huchemshwa au kuchomwa kwa maombi ili kufukuza mapepo waliojificha kwenye miti au maeneo ya nyumba.


✅ 4. Kutuliza Roho za Mizimu au Miiko ya Ukoo

Katika baadhi ya koo, mwembe huaminika kuwa na roho ya ukoo.
๐Ÿช” Kwa watu wanaofuatwa na mizimu, kuchukua majani ya mwembe na kufanya maombi ya kukana maagano ya mizimu hutuliza nguvu za kurithi roho chafu.


✅ 5. Moto wa Mwenyezi Mungu Juu ya Madhabahu za Giza

Katika maombi ya vita, mtu anaweza kuinua mikono juu ya mwembe aliowahi kuona kwenye ndoto na kutangaza:

“Moto wa Mwenyezi Mungu ushuke juu ya kila mwembe ulio madhabahu ya giza kwenye ukoo wangu!”


๐Ÿ“– Maandiko ya Msingi:

  • Isaya 49:25 – “Lakini Mwenyezi Mungu asema hivi: Nitamwokoa mwenye nguvu mateka yake...”
  • Luka 10:19 – “Nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge, na kushinda nguvu zote za adui...”

๐Ÿ“Œ Imeletwa na Dr Magowo
๐Ÿ“ Fuata: Angaza Nuru

No comments:

Post a Comment