Tuesday, November 12, 2024

KUSAFISHA NYOTA NA KUFUNGUA CHAKRA YAKO.

KUSAFISHA NYOTA NA KUFUNGUA CHAKRA YAKO. Endapo wewe mtaalamu wa tiba unahitaji kumfungua na kumsafisha mteja au kuwasafisha wateja wako wawe na mvuto na nyota zao zing'ae basi tumia dawa hizi pamoja na njiwa mweupe hapa tunatumia damu ya vidole utachanganya na dawa za kumfungua mteja huyo . Kata kidole cha kati cha njiwa mweupe kisha ile damu dondoshea kwenye mchanganyiko wa dawa nitakazo kutajia hapa chini. Mocha ngoko Mkanya Mtegua Vifungo Muosha Fedha Mwenda Mkulungu Nyahinga Mpasua Jabari Mkoba shengelo. Dawa hizo zote zichanganye kisha utadondoshea damu ya njiwa mweupe ambaye hana doa. Changanya kwa pamoja ikisha changanyika utakwenda kumuosha mgonjwa na kama wewe sio mtaalamu lakini unataka kufungua nyota yako na vifungo vyako kwa kutumia dawa hii basi utafanya kama nilivyo elekeza hapa utanunua na kitambaa cheupe mita moja utajifunga wakati unaoga huo mchanganyiko. Ukisha tumia damu ya njiwa huyo utamwachia njiwa aende kama uliifanya kazi hiyo ukiwa ndani basi toka nje kisha umrushe aende nuwia kung'arisha nyota yako na kufungua ridhiki zako,kwenye biashara au kwenye kazi zako pamoja na kusikilizwa na kila mtu.

No comments:

Post a Comment