Tuesday, November 12, 2024

FAHAMU FAIDA ZA MCHAICHAI KWA AFYA

FAHAMU FAIDA ZA MCHAICHAI KWA AFYA 1.Husaidia kusafisha figo na mkojo. Mchaichai pia una kazi ya kusafisha figo ambayo kazi yake ni kusafisha damu mwilini, kuondoa mafuta mabaya mwilini ambayo mengi yanatengenezwa na kemikali za kiwandani na hivyo mwili kushindwa kuziondoa na baadaye kusababisha magonjwa mbalimbali ikiwemo Saratani na matatizo ya figo. 2.Hupunguza maumivu wakati wa hedhi, Mchaichai pia husaidia wanawake ambao wanaumwa na tumbo kipindi cha hedhi ambao wengi wao huchukulia kama chango. Unapokunywa Mchaichai unaweza kusafisha mirija ya uzazi na hivyo kuwezesha damu kupita kwa urahisi". 3.Mchaichai husaidia kutibu vidonda vya tumbo. 4.Mchaichai ni kinga dhidi ya Saratani. Tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa kwenye kila gramu 100 ya Mchaichai kuna viondosha sumu ambavyo vina uwezo wa kuulinda mwili dhidi ya ugonjwa wa Saratani. 5.Hutibu magonjwa ya kuhara, husaidia mmeng'enyo wa chakula. Chai ya Mchaichai hurahisisha utaratibu wa mmeng'enyo wa chakula na pia hutibu magonjwa ya kuhara na maumivu ya tumbo ikiwemo tumbo kujaa gesi. 6.Hurahisisha utaratibu wa kuondoa uchafu mwilini. 7.Hushusha joto la mwili pale linapokuwa limepanda, hivyo kushusha homa huku mgonjwa akiendelea na dawa.

No comments:

Post a Comment